Biashara ya muziki.
Mwaka 2004 niliandika kitabu kuhusu biashara ya muziki. Kwa
wakati huo kitabu hicho “Introduction To Music Business”
kilishabihiana na mazingira ya wakati huo.
Miaka michache iliyopita, dunia ilitegemea mabadiliko
makubwa kwenye biashara ya muziki kutokana na kuingia kwenye mfumo wa dijitali
(digital). Upatikanaji wa bidhaa za muziki kupitia mtandao wa intaneti, ilikuwa
furaha kwa mtumiaji. Na urahisi wa kupata wimbo mmoja badala ya kununua toleo
lote la albamu fulani, na kwa gharama nafuu.
Katika suala la uchumi kwenye biashara ya muziki ni kipigo
kwa msanii. Labda kwa wasanii wakubwa na wenye uwezo wa kulazimisha mkataba
wenye makato ya juu.
Kwa uhalisia, kampuni ya uaandaji wa muziki ‘lebo’ – ni
mwekezaji. Unapokuwapo mkataba; lebo inabeba gharama za kurekodi, kusambaza na
kuitambulisha pia. Lebo inafanya hivyo kwa makubaliano ya makato kutoka kwenye
mauzo. Na huo ndio mfumo ulivyo, hadi
tulipofikia mfumo wa kidijitali.