Baada ya ongezeko la timu kutoka 16 hadi 24 Cameroon ilishiriki kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia 1982 huko Hispania. Pamoja na kutokufungwa kwao walishindwa kufuzu kuingia mzunguko wa pili. Roger Milla, mchezaji maarufu Afrika; alishiriki kwa mara ya kwanza pia.
Kombe la Dunia 1990, timu ya taifa ya Cameroon ikiwa na François Omam Biyik ambaye aliwazamisha mabingwa watetezi Argentina 1-0 katika mechi ya ufunguzi. Mechi ambayo iliweka historia katika mashindano ya Kombe La Dunia. Katika mechi ya pili, timu ya taifa ya Cameroon iliibwaga Romania mabao 2-1; huku Roger Milla akifunga mabao yote kwa timu yake. Kufungwa 4-0 na Umoja wa Kisovieti, timu ya taifa ya Cameroon ilikuwa imekwishafuzu kuingia mzunguko wa pili.
Katika mzunguko huo wa pili Cameroon iliitandika timu ya taifa ya Colombia 2-1 - wakati Roger Milla aliyekuwa na umri wa miaka 38 kufunga mabao mawili katika muda wa ziada.
Katika hatua ya robo fainali Cameroon walikabiliwa Uingereza. David Platt alifunga katika dakika ya 25 kwa upande wa Uingereza. Katika nusu ya pili hata hivyo, Cameroon alirudisha bao katika dakika 61 - penati kutoka kwa Emmanuel Kundé, huku Eugène Ekéké akipachika bao katika dakika ya 65. Hata hivyo, Uingereza walipata penati katika dakika ya 83 na Gary Lineker kufunga bao la kusawazisha. Lineker alifanya hivyo hivyo katika dakika ya 105 na kupata penati iliyoipa Uingereza ushindi kwa mabao 3-2.
Kombe la Dunia 1994 nchini Marekani, Roger Milla alicheza katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Urusi. Akiwa na umri wa miaka 42 - Roger Milla akawa mchezaji kongwe kucheza na kufunga katika mechi za Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment