Sunday, June 15, 2014

Kombe La Dunia 2014 - Ndio matokeo.


Pamoja na kuonyesha kandanda safi ya kushambulia, timu ya taifa ya Uingereza ilionekana kama ilitaka kuanzisha aina tofauti na mpya kabisa ya kusakata soka kwa nchi hiyo. Ni mchezo tofauti na wengi walivyozoea kuiona timu hiyo inacheza. Lakini, kocha na wachezaji wanayo haki ya kuwa na faraja na uchezaji wao - ukiangalia jinsi timu ilivyochangia kwenye usiku mahiri wa kandanda ya kushambulia. Je, ni makosa ambayo yalisababisha kupoteza mechi, au ukubwa wa mechi ndio ulichangia?

Katika kulinda goli la Mario Balotelli, beki wa kushoto wa timu ya Uingereza Leighton Baines hakuwa karibu na Antonio Candreva kuzuia krosi na Gary Cahill alimsahau nyuma Balotelli na kumpa nafasi ya kupiga kichwa na kufunga. Kwa kuzingatia kuwa Uingereza wamepoteza mechi ya ufunguzi, njia ya kuondoka katika Kundi D inaonekana na madhara zaidi.
Habari zilizojitokeza masaa machache kabla ya mchezo kwamba kijana machachari wa timu ya Liverpool atapangwa, zilipokelewa kwa furaha na wachambuzi mbali mbali - na ulikuwa uamuzi sahihi. Kijana alifanya mambo yake, na aliionya Italia kwa tishio lake wakati alipokimbia kwa kasi kama risasi na kupiga shuti lililopiga nyavu ndogo, wengi ndani ya uwanja waliamini alikuwa amefunga. Ndiyo, alipoteza milki mara chache lakini Raheem Sterling alionyesha hawaogopi wapinzani. Kiwango chake kimemuhakikishia nafasi dhidi ya Uruguay.




Timu ya taifa ya Italia iliondoka na furaha kubwa kutokana na ushindi dhidi ya Uingereza. Katika mechi ile, timu ya Italia ilitumia nafasi kuionyesha dunia umahiri wa vipaji vyake.
Daima alichukuliwa kama mchezaji mwenye uwezo, Antonio Candreva ameibuka kama moja ya viungo wa hali ya juu katika miaka miwili. Kabla ya kuwasili kwake  Lazio, alikuwa mchezaji wa kawaida kule Cesena. Umahiri wa Candreva pale Lazio na kipaji chake ndio vimempa nafasi katika Azzurri.

No comments:

Post a Comment