Thursday, June 19, 2014

Red Card - Ipo kwenye damu.


Kwenye familia ya wanasoka huko Cameroon - 'Familia ya SONG' (Rigobert na Alex), kitende cha kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi za Kombe La Dunia ni kama kuonyeshwa zawadi wakati wa sherehe. Ni vigumu kupata au kutoa maelezo ya vitendo vya wanafamilia hao; zaidi ya kujiuliza maswali. "Alex, kwa nini ulifanya vile?"




Kutolewa nje kwa Song mwenye umri wa miaka 26 - kumefuatiwa msimu kuwakatisha tamaa kwa Song huko Hispania ambapo ameonekana/amecheza kwa muda mdogo katika msimu wa pili tangu kuhama kutoka Arsenal na kwenda Barca. Kama ni kuhama, anaweza kupata mnunuzi?




Maswali ni mengi, lakini anaonyesha nyayo za mjomba wake Rigobert alipata kadi nyekundu katika mashindano ya mwaka 1994 na 1998. Kutokana na kadi hiyo nyekundu, Alex na Rigobert wameonyeshwa kadi nyekundu tatu kati ya nane ambazo timu ya taifa ya Cameroon imeonyeshwa katika mashindano ya soka ya Kombe La Dunia.
  
 
Massing alivyomrusha Cannigia. Italia '90.

 
Rigobert Song



Alex Song




No comments:

Post a Comment