Thursday, June 12, 2014
Kombe La Dunia - Brazil 2014
Leo yanaanza mashindano ya mpira wa miguu - Kombe La Dunia 2014. Wengine bado wana kumbukumbu za mashindano yaliyopita yaliyofanyika Afrika ya Kusini 2010.
Pamoja na kutazama vivutio vya mashindano hayo. Nitaandika nitakachoona kwa macho yangu, nitaandika nitakayosikia kwa masikio yangu; pia nitachambua yale ambayo nitakayosoma.
Kombe la Dunia 2014 litakuwa na mvuto pekee kutokana na mabadiliko mengi, hasa katika kizazi cha sasa. Teknolojia imesambaa duniani kote, wapenzi wa mpira wa miguu wanaweza kufuatilia maendeleo, habari na matukio ya mchezo wa soka kwa urahisi.
Jambo lingine linaloleta mvuto ni nchi ambayo mashindano hayo yanafanyika - Brazil. Nchi inayotambulika kwa vipaji na uwezo wa soka duniani. Pamoja na hayo, mpira wa miguu ulipelekwa katika nchi hiyo na mtu aliyeitwa Thomas Donohue.
Kivutio kingine ni wale nyota wa mchezo huu - hivi sasa wapo nyota wengi na wenye kiwango na uwezo wa hali ya juu, ambao wanacheza soka katika ligi kubwa duniani na kulipwa mishahara ya juu.
Ni nyota gani itang'ara na kuliwezesha taifa lake kubeba Kombe La Dunia?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment