Friday, May 3, 2013

Killi Awards 2013


Kupitia mitandao ya kijamii na hata baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini, imeonyesha jinsi Watanzania walivyoshiba tabia kulalamika. Sina maana kuwa ni wananchi wote wanayo hiyo tabia, ila ni baadhi. Pia kutokana na kuwapo uhuru wa kujieleza kwa kuandika au hata kuongea, wengi tumekuwa wepesi kutumia nafasi hiyo.
Angalia matokeo ya mitihani ya kidato cha nne - nadhani kila mtu alikuwa na maoni na mtazamo wake. Sio mbaya hata kidogo. Lakini asilimia kubwa ilikuwa ni malalamiko, labda kutokana na mfumo, ufisadi, wazazi n.k. Upande mwingine walitokea waliojenga mtazamo wa ufumbuzi wa tatizo kwa ajili ya vizazi vinavyokuja. Fuatilia mchakato wa Katiba, mvutano wa hisia ni mkali.
Sasa kuna hizi tuzo za muziki - zinapata mashambulizi badala ya kushauri pale kwenye mapungufu.

Kwa nini kuchunguza/kufuatilia choo cha jirani?

No comments:

Post a Comment