Tarehe 4 Mei 2013 International Reggae And World Music Awards (IRAWMA) walimtangaza Kevin Wyre kama 'Best New Entertainer' kwenye tuzo zao ambazo zilianzishwa mwaka 1982.
Kenya itakuwa na furaha na haki zote za kujivunia mafanikio ya Wyre, maana amekuwa mwakilishi wa muziki na wasanii wa nchi hiyo katika anga za kimataifa. Pia ni sifa kwa Afrika Mashariki kupata mwakilishi katika dunia ya muziki ambayo imetawaliwa na wasanii wakubwa kutoka Amerika na Ulaya.
Kushindana na wasanii wakubwa wenye kufahamika ambao wanapata msaada kutoka kwa kampuni na vikundi vingine kwenye dunia ya muziki - ni kitu cha kujivunia. Hivi sasa ukitaja Chronixx, basi hilo ndio jina lililopo mdomoni kwa wengi wanaofuatilia muziki kutoka Jamaica. Ni msanii ambaye yupo katika nafasi ya juu kwenye muziki wa dancehall.
Wyre kwa hivi sasa anasikika kwenye riddims (midundo) mpya za muziki wa dancehall. Ni msanii mwenye mvuto wa kimataifa. Nitakuwa mchoyo kama sitaeleza furaha kubwa niliyokuwa nayo kuona mafanikio ya Wyre.
Nitamtaja Ted Josiah maana kupitia yeye ndio nilipoona kuwa kipaji cha Wyre kinaelekea kwenye mafanikio. Wakati huo alikuwa kwenye kikundi cha Necessary Noize (wengine kwenye kikundi walikuwa Nazizi na Bamzigi). Wakati tukiwa na East Africa Radio - pamoja na Sista Dread tulishirikiana kuandaa ziara ya Necessary Noize kuja kujitangaza hapa Tanzania.
Baada ya hapo Wyre, Bebe Cool na Nazizi waliungana kuunda East Africa Bashment Crew - ambao walisaidia kuinua na kuleta mabadiliko katika muziki wa Afrika Mashariki.
Ushirikiano na wasanii wengine wa muziki wa dancehall unaonyesha njia ambazo Wyre amepiatia.
HONGERA WYRE!!!
No comments:
Post a Comment