Saturday, May 4, 2013

Vijana wa leo.

 Wakati wa utoto kwenye miaka ya sabini, tuliwaangalia kaka zetu na dada zetu (hata wajomba na shangazi zetu) walivyohangaika kukimbia na kujificha kutoka kwa wazazi na watu wazima ambao walikuwa wanawakalia kooni kutokana na tabia zao. Ilipofika wakati wetu, ambayo ni miaka ya themanini, tulihisi na kujiona kuwa tumebanwa sana na wakubwa wetu. Mzunguko huo ni wa vizazi, wataalamu wa tabia za jamii wanaweza kufafanua kutokana ufahamu wao.


Nimekuja kutambua kuwa - mazingira ya namna hiyo yanatokana na kukosekana 'daraja' la mawasiliano. Na pande zote mbili zinazovutana zinayo majukumu ya kutekeleza kusudi kupata uwanja wa pamoja, pale kwenye uelewano usioelemea upande wowote. Wakubwa wanakuwa wamejaliwa ufahamu wakati wadogo wanakuwa na ufahamu finyu kidogo. Kwahiyo, huo ni mvutano wa ufahamu.


'Msiwalaumu vijana, wala msituchukulie kama wajinga.' Ni maneno yaliyotamkwa na vijana wa Musical Youth kwenye wimbo wao unaoitwa 'The Youth Of Today' zaidi ya miaka thelathini iliyopita. Walichokuwa wanaeleza ni kuwa sisi ni vijana wa leo, inabidi tuishi kama vijana wa leo. Na kawaida kama vijana wakiingiliwa katika maisha yao, lazima watatetea mazingira yao na hata kufanya mapinduzi kuhalalisha ufahamu wao. 'Huu ni wakati wa hukumu.'




No comments:

Post a Comment