Friday, June 20, 2014
Thursday, June 19, 2014
Red Card - Ipo kwenye damu.
Kwenye familia ya wanasoka huko Cameroon - 'Familia ya SONG' (Rigobert na Alex), kitende cha kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi za Kombe La Dunia ni kama kuonyeshwa zawadi wakati wa sherehe. Ni vigumu kupata au kutoa maelezo ya vitendo vya wanafamilia hao; zaidi ya kujiuliza maswali. "Alex, kwa nini ulifanya vile?"
Kutolewa nje kwa Song mwenye umri wa miaka 26 - kumefuatiwa msimu kuwakatisha tamaa kwa Song huko Hispania ambapo ameonekana/amecheza kwa muda mdogo katika msimu wa pili tangu kuhama kutoka Arsenal na kwenda Barca. Kama ni kuhama, anaweza kupata mnunuzi?
Maswali ni mengi, lakini anaonyesha nyayo za mjomba wake Rigobert alipata kadi nyekundu katika mashindano ya mwaka 1994 na 1998. Kutokana na kadi hiyo nyekundu, Alex na Rigobert wameonyeshwa kadi nyekundu tatu kati ya nane ambazo timu ya taifa ya Cameroon imeonyeshwa katika mashindano ya soka ya Kombe La Dunia.
Massing alivyomrusha Cannigia. Italia '90.
Rigobert Song
Alex Song
Monday, June 16, 2014
Kombe La Dunia 2014: Hii itakuwa mechi ya kuangalia!
Ureno v Ujerumani (Group G)
Ujerumani na Ureno ni mataifa mawili ambayo yapo katika nafasi tano za juu katika viwango vya FIFA, na wote wana uwezo wa kufanya maajabu katika Kombe la Dunia 2014.
Ureno ni timu ngumu kuitabiri. Walihitaji mchujo kupata ushindi dhidi ya Sweden kufikia fainali za Kombe la Dunia. Walipoteza mchezo mmoja tu katika kufuzu, lakini walifungwa na Israel mara mbili.
Suala kubwa kwa Ureno wiki chache zilizopita limekuwa afya ya nyota wao Christiano Ronaldo. Amekuwa akikabiliana na tatizo kwenye mguu. Ronaldo ana uwezo wa kubeba mafanikio yao, ila tatizo lao kidogo limekuwa ni ukosefu wa mshambuliaji wa kati, lakini pembeni wamekamilika.
Kwa upande mwingine, Ujerumani wamejikuta wanashughulika na majeruhi mengi. Marco Reus atakosa mashindano kutokana na kuumia kifundo cha mguu. Kipa Manuel Neuer ni mmoja wa makipa bora dunia, lakini alikuwa uliumia bega. Yeye atacheza. Kiungo Bastian Schweinsteiger aliumia goti mwezi uliopita, lakini yeye pia anatarajiwa kuwa fit.
Ujerumani ni moja ya taifa linalotarajiwa kushinda mashindano haya. Walikuwa moja ya timu zilizofanya vizuri zaidi katika kufuzu, kwa kushinda michezo tisa na kutoka sare moja, na kufunga mabao 36 katika mechi 10.
Hizi ni timu mbili bora katika dunia, na Ujerumani kati ya timu zinazitarajiwa kunyakua Kombe la Dunia 2014; bila kusahau kuwa Ureno ina mchezaji bora duniani - Ronaldo.
Ngamia ametabiri mshindi!!
Sunday, June 15, 2014
Kombe La Dunia 2014 - Ndio matokeo.
Pamoja na kuonyesha kandanda safi ya kushambulia, timu ya taifa ya Uingereza ilionekana kama ilitaka kuanzisha aina tofauti na mpya kabisa ya kusakata soka kwa nchi hiyo. Ni mchezo tofauti na wengi walivyozoea kuiona timu hiyo inacheza. Lakini, kocha na wachezaji wanayo haki ya kuwa na faraja na uchezaji wao - ukiangalia jinsi timu ilivyochangia kwenye usiku mahiri wa kandanda ya kushambulia. Je, ni makosa ambayo yalisababisha kupoteza mechi, au ukubwa wa mechi ndio ulichangia?
Katika kulinda goli la Mario Balotelli, beki wa kushoto wa timu ya Uingereza Leighton Baines hakuwa karibu na Antonio Candreva kuzuia krosi na Gary Cahill alimsahau nyuma Balotelli na kumpa nafasi ya kupiga kichwa na kufunga. Kwa kuzingatia kuwa Uingereza wamepoteza mechi ya ufunguzi, njia ya kuondoka katika Kundi D inaonekana na madhara zaidi.
Habari zilizojitokeza masaa machache kabla ya mchezo kwamba kijana machachari wa timu ya Liverpool atapangwa, zilipokelewa kwa furaha na wachambuzi mbali mbali - na ulikuwa uamuzi sahihi. Kijana alifanya mambo yake, na aliionya Italia kwa tishio lake wakati alipokimbia kwa kasi kama risasi na kupiga shuti lililopiga nyavu ndogo, wengi ndani ya uwanja waliamini alikuwa amefunga. Ndiyo, alipoteza milki mara chache lakini Raheem Sterling alionyesha hawaogopi wapinzani. Kiwango chake kimemuhakikishia nafasi dhidi ya Uruguay.
Timu ya taifa ya Italia iliondoka na furaha kubwa kutokana na ushindi dhidi ya Uingereza. Katika mechi ile, timu ya Italia ilitumia nafasi kuionyesha dunia umahiri wa vipaji vyake.
Daima alichukuliwa kama mchezaji mwenye uwezo, Antonio Candreva ameibuka kama moja ya viungo wa hali ya juu katika miaka miwili. Kabla ya kuwasili kwake Lazio, alikuwa mchezaji wa kawaida kule Cesena. Umahiri wa Candreva pale Lazio na kipaji chake ndio vimempa nafasi katika Azzurri.
Saturday, June 14, 2014
Fatou
Mwimbaji wa Mali, Fatoumata Diawara (aka Fatou) alizaliwa nchini Ivory Coast mwaka 1982 kisha kulelewa katika nchi ya Mali.
Akiwa na umri wa miaka kumi na nane, Fatou alisafiri hadi Paris (Ufaransa) kufanya maonyesho. Baada ya ziara, Fatou alirudi Mali ambapo mwaka 2001 alicheza filamu inayoitwa 'Sia'. Kwa wengi katika nchi za Mali, Guinea, Senegal na Burkina Faso; Fatou kwao ni Sia - shukrani kwa mafanikio ya filamu hiyo.
Ukurasa wa Fatou.
Kombe La Dunia 2014 - Costa Rica kuwatuma mashujaa wao.
Edinson Cavani yupo tayari kubeba mzigo kutokana na kukosekana kwa Luis Suarez kwa Uruguay kwenye mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia 2014. Suarez alikuwa kwenye matibabu ya goti lake la kushoto.
Uruguay walimaliza nafasi ya nne miaka minne iliyopita kule Afrika Kusini, mchango mkubwa ulitokana na magoli matano ya Diego Forlan, ambayo yalimwezesha kupata heshima ya mpira wa dhahabu. Sasa Uruguay itakutana na Costa Rica katika mechi yao ya kwanza.
Costa Rica itawatuma mashujaa wao wa mabao, pamoja na kiungo Bryan Ruiz, ambaye amepachika mabao 12 katika mechi 63 tangu mwaka 2005. Atakayekuwapo pamoja na Ruiz ni Joel Campbell mwenye umri wa miaka 21 - ambaye wakati wa mzunguko wa kufuzu, Campbell pia alipachika bao moja katika mechi tano.
Friday, June 13, 2014
VIDEO: Biggaton "Crime Stopper"
Kevin Roye 'Biggaton' alizaliwa Aprili 17 na kukulia huko Mandeville. Yeye alihudhuria shule ya Mandeville, kutoka ambapo alipata udhamini kwenda chuo cha Ufundi Holmwood High. Alianza deejaying wakati akiwa Holmwood High kwa msaada wa rafiki zake.
Soma Zaidi kuhusu Biggaton.
Kombe La Dunia 2014 - GHANA
Asamoah Gyan alifunga goli dhidi ya Korea Kusini na katika kushangilia, wachezaji wa timu ya taifa ya Ghana wakajikita katika Azonto, ngoma maarufu kutoka Ghana.
Ushindi dhidi ya timu ya Marekani miaka minne iliyopita uliipeleka timu ya taifa ya Ghana katika robo fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza. Ghana ulikubalika kama "Timu ya Afrika" - ilitegemewa kuwa nchi ya kwanza kutoka Afrika kufikia nusu fainali, lakini kupoteza mechi kwa Urugwai kwa mikwaju ya penati; safari ilikomea hapo.
Waghana wanayo kila sababu ya kuwa na matumaini, kwa sababu ya kuweza kuwaondoa Marekani katika mashindano mawili mfululizo ya Kombe la Dunia. Basi itabidi tujitayarishe kwa Azonto nyingine.
Thursday, June 12, 2014
"You can jail a Musician, but you can't jail the Music". - Vitali Maembe
Vitali Maembe:
"Alhamisi
tarehe 12 jioni ntakuwa na watoto wa mitaani maeneo ya kariakoo. Ijumaa
Tarehe 13 asubuhi nitatembelea Mahabusu ya watoto Dar, Mchana naanza
kuelekea Bagamoyo kwa miguu, njiani nitapiga muziki na kujadili na watu
juu ya elimu. Jmosi tarehe 14 na Jpili Tarehe 15 nitakuwa njiani. Jtatu
Tarehe 16 nitapokewa na wanamuziki wengine tutajumuika pamoja Bagamoyo
kupaaza sauti zetu juu ya umuhimu wa Elimu kwa watoto wote."
Muziki wa Reggae unakufa?
Kwa miaka takriban kumi, muziki wa Reggae umesambaa kwa kasi katika kona nne za dunia. Teknolojia imechangia sana katika mabadiliko yaliyotokea - kuanzia kwenye uandishi, midundo na utamaduni unaoambatana na muziki huo.
Yupo mwandishi mmoja anaitwa Davina Hamilton wa huko Uingereza, amewahi kuuliza kama 'Muziki wa Reggae Umekufa?'. Katika makala yake, alihojiana na wadau tofauti; ambao walifafanua kutokana na mazingira yao. Mwandishi huyo wa habari za burudani, alirudia tena kuandika 'Kifo cha polepole' na kumalizia kwa kuandika kuwa muziki wa Reggae umetawala sana na kuzoeleka katika mfumo uliopo, ndio maana hakuna mtu anayegundua kuwa bado unaishi. Kwa maana, umekuwa wa kawaida sana.
Takwimu za mauzo katika nchi za Marekani na zile za Ulaya zinaonyesha kushuka sana kwa mauzo ya santuri za Reggae. Utafiti kuhusu uhudhuriaji wa wapenzi wa muziki huo, unatofautiana kwa sehemu mbali mbali. Pamoja na mijadala ambayo imetokea, maswali bado yanaulizwa. Angus Taylor (mwandishi) anataka kujua kuhusu kushuka kwa mauzo - 'Inamaanisha nini?.
"Hatutarudi nyuma kulinda." - Asema Modric.
Luka Modric ni kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Croatia ambaye anacheza Real Madrid ya Hispania, ametamka wazi kuwa timu ya taifa ya Brazil ndio wanaoonekana kuwa watachukua Kombe La Dunia mwaka huu. Lakini ametahadharisha kuwa hawataingia uwanjani kwa uwoga, lakini watapambana na vigogo hao katika mechi ya ufunguzi wa Kombe La Dunia 2014.
"Itakuwa kazi nzito katika kiungo na sisi tutapotea kama tukijisalimisha na kujaribu kukaa nyuma na kulinda."
Kombe La Dunia - Brazil 2014
Leo yanaanza mashindano ya mpira wa miguu - Kombe La Dunia 2014. Wengine bado wana kumbukumbu za mashindano yaliyopita yaliyofanyika Afrika ya Kusini 2010.
Pamoja na kutazama vivutio vya mashindano hayo. Nitaandika nitakachoona kwa macho yangu, nitaandika nitakayosikia kwa masikio yangu; pia nitachambua yale ambayo nitakayosoma.
Kombe la Dunia 2014 litakuwa na mvuto pekee kutokana na mabadiliko mengi, hasa katika kizazi cha sasa. Teknolojia imesambaa duniani kote, wapenzi wa mpira wa miguu wanaweza kufuatilia maendeleo, habari na matukio ya mchezo wa soka kwa urahisi.
Jambo lingine linaloleta mvuto ni nchi ambayo mashindano hayo yanafanyika - Brazil. Nchi inayotambulika kwa vipaji na uwezo wa soka duniani. Pamoja na hayo, mpira wa miguu ulipelekwa katika nchi hiyo na mtu aliyeitwa Thomas Donohue.
Kivutio kingine ni wale nyota wa mchezo huu - hivi sasa wapo nyota wengi na wenye kiwango na uwezo wa hali ya juu, ambao wanacheza soka katika ligi kubwa duniani na kulipwa mishahara ya juu.
Ni nyota gani itang'ara na kuliwezesha taifa lake kubeba Kombe La Dunia?
Subscribe to:
Comments (Atom)





















